28 Oktoba 2026 - 22:53
Mufti Mkuu wa Tanzania Asaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kidini kati ya BAKWATA na Urusi

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zuber bin Ali, asaini mkataba wa ushirikiano wa kidini kati ya BAKWATA na taasisi za masuala ya dini za Urusi, tarehe 27 Oktoba 2026, nchini Urusi, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kidini, amani na maendeleo kati ya Tanzania na Urusi.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s.) -ABNA- Sheikh Dkt. Abubakar Zuber bin Ali, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, amesaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa kidini kati ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) na taasisi za masuala ya dini za Shirikisho la Urusi.

Mkataba huo ulisainiwa tarehe 27 Oktoba 2026, nchini Urusi, katika hafla iliyohusisha Sheikh Ravil Gaynetdin, Mufti Mkuu wa Urusi, na Sheikh Abubakar Zuber, Mufti Mkuu wa Tanzania.

Makubaliano hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano katika masuala ya kidini kati ya BAKWATA na upande wa Urusi, huku yakifungua fursa za kuendeleza mawasiliano na kubadilishana uzoefu katika shughuli za kidini.

Katika ziara yake ya kidini nchini Urusi, Mufti Mkuu wa Tanzania pia alishiriki Kongamano la Kimataifa kuhusu madaraja ya juu ya kiroho kati ya Urusi na Afrika, pamoja na mazungumzo yanayohusu amani na maendeleo.

Ziara hiyo na utiaji saini wa makubaliano hayo vinaweka msingi wa kuendeleza mawasiliano kati ya taasisi za kidini za Tanzania na Urusi, hususan katika maeneo ya ushirikiano wa kidini, mazungumzo na juhudi za kukuza amani na maendeleo.

Mufti Mkuu wa Tanzania Asaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kidini kati ya BAKWATA na Urusi

Mufti Mkuu wa Tanzania Asaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kidini kati ya BAKWATA na Urusi

Mufti Mkuu wa Tanzania Asaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kidini kati ya BAKWATA na Urusi

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha